Thursday, March 25, 2010

Ajali iliyotokea leo alfajiri kibamba

Watu saba waliokuwa kwenye Hiace wamefariki hapo hapo baaada ya lori la mafuta lililokuwa linatoka Dar kwenda pwani kuigonga hiace na kuiburuza hadi mtaroni ambapo iliilalia.


Hakuna hata mmoja aliyetoka kama unavyoona kwenye picha.



Ni maiti mbili tu zikiwa vipande ndo zimetolewa na zingine bado maana kazi ya kulitoa hilo lori ngumu ukizingatia lina petroli.
Wafiwa wote poleni sana na waliofikwa na umauti Mungu awarehemu. Amen.

2 comments:

  1. Jinsi Hiace hiyo ilivyopondeka, ni ajabu kusikia kwamba kuna watu wamenusurika kama ilivyoripotiwa kwa Michuzi. Mungu Awapumzishe salama waliopoteza maisha yao. Wameondoka nyumbani salama wakiwahi kwenye mihangaiko yao ya siku na ghafla kifo kikapiga hodi. Inasikitisha sana!

    ReplyDelete
  2. nasikia kusisimuka juu ya hii ajali , Ewe mola Wapokee wale wote waliotangulia mbele ya haki. Amen

    ReplyDelete